Wizara ya Nishati na madini ofisi ya kahama Mkoani Shinyanga imesema kuwa zoezi la uopoaji wa miili ya watu saba ya katika shimo la mgodi wa Nyangarata huenda likachukua miezi 3 kuwafikia kutokana kuwa kampuni ya Mgodi wa ACACIA Bulyanhuru kukataa kutoa vifaa vya kuchimbilia eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofsini kwake kaimu kamishina wa migodi katika wizara hiyo wilayani Kahama Robert Nyasili amesema kuwa zoezi hilo litachukua muda mrefu kutokana kuwa wachimbaji wa eneo hilo ndio watakaotumika katika kufukua miili hiyo.
Amesema kuwa mgodi wa Bulyanhulu ulishindwa kutoa vifaa kutokana kuhofia usalama wa vifaa na usalama wa wafanyakazi kwa kuwa eneo hilo linatitia hivyo linaweza kusababisha maafa zaidi ya yaliyojitokeza.
Aidha amesema kuwa wachimbaji wadogo wamelazimika kuchanga fedha kwa ajili ya kukodi mitambo isiyo na uzito ili kusaidia kuchimba kidogo kidogo na kwa sababu eneo walilofukiwa watu lipo kina kirefu hivyo zoezi hilo linaweza kuchukua miezi 3 hadi minne.
Mnamo tarehe 5 mwezi huu Machimbo ya Dhahabu ya Nyangarata yaliyopo kata ya Lunguya wilayani Kahama yalititita chini na kufukia watu 7 na wengine 10 wakiopolewa wakiwa hai yanaelezwa chanzo chake kuwa ni mfumo duni wa uchimbaji ambao ulikuwa unatekelezwa na wachimbaji wadogo wadogo machimboni hapo.
No comments:
Post a Comment