Tuesday, October 13, 2015

DIAMOND PLATNUMZ AMPA ROSE NDAUKA ZAWADI YA KEKI KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA.

NDAUKA (5)Rose akipewa zawadi ya keki na Harmonizer kwa niaba ya Wasafi Classic Baby.
Stori: Brighton Masalu
na Musa Mateja
KUPITIA baadhi ya vijana walio chini ya kundi lake la Wasafi Classic Baby (WCB), ‘kichaa’ wa Bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amepelekea zawadi ya keki, staa wa filamu za Kibongo, Rose Donatus Ndauka alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.
NDAUKA (4)Msanii chipukizi wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WBC’ aitwaye Harmonizer akilishwa keki na Rose.
Ishu hiyo ilijiri Jumatano iliyopita ndani ya Ukumbi wa Jozi Village, Msasani jijini Dar ambapo vijana hao wa Diamond wakiongozwa na msanii ambaye anasimamiwa muziki na Diamond, Hamonizer, walitinga ukumbini hapo wakiwa wameshikilia boksi lililokuwa na keki, maalum kwa ajili ya Rose.
NDAUKA (3)Oscar Ndauka akilishwa keki na Rose Ndauka ambaye ni mtoto wa kaka yake
Muda wa kula keki
ulipowadia, mbali na rafiki wengine kumuandalia muigizaji huyo keki, Kundi la Wasafi Classic Baby lilifunua keki yao ikiwa na maandishi ya ‘Happy Birthday Rose Ndauka, from Wasafi Classic Baby (WCB)’ ambapo walianza kumlisha huku minong’ono na miguno ikianza kusikika miongoni mwa wageni waalikwa.
Baadhi ya maneno na fununu ambazo zilitawala ukumbini humo ni kuwa zawadi hiyo ya keki iliandaliwa na Diamond ambaye kwa sasa ni mtu wake wa karibu lakini hapendi watu wajue ndiyo maana akawatuma Wasafi wamuwakilishe sambamba na dada yake, Darleen Abdul ‘Queen Darleen’.
Baada ya tukio hilo, waandishi wetu ‘walimbananisha ukutani’ Rose kwa lengo la kutaka kujua lipi ni ‘tui na yapi ni maziwa’ juu ya madai hayo, aling’aka na kusema yeye na Diamond ni marafiki hivyo si ajabu kuona vijana wake wakimletea zawadi.
“Jamani, mbona tunafuatiliana sana? Kwani mimi kupewa keki na vijana wa Diamond ni tatizo? Hii ni sherehe, mtu yeyote hata nyinyi mnaweza kunipa zawadi, niacheni nifurahie kuzaliwa kwangu,” alisema Rose.
Sherehe hiyo iliyofana vilivyo kwa watu kunywa na kula, mastaa mbalimbali walihudhuria akiwemo Jacqueline Wolper, Hamisa Mobeto na prodyuza, Emmanuel Sewando ‘Manecky’

No comments: