Saturday, October 17, 2015

MAGUFURI AKIMWAGA SELA NDANI YA ZANZIBAR.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa  visiwa vya Unguja kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisisitiza kuulinda Muungano na kuwaambia kuwa atazifanyia kazi kero zilizobaki za Muungano.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
Makamu wa Rais wa Dk.Gharib Bilal akihutubia wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaombea kura Dk. John Pombe magufuli pamoja na Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Hassan Mwinyi akihutubia kwenye mkutano wa kampeni zakuwanadi wagombea wa nafasi za urais kupitia CCM .
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuhutubia wananchi na wanaCCM waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM Uliofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Sheta akitoa burudani kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja.

No comments: