Hatari! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma anadai kutishiwa maisha
kwa kutumiwa ujumbe wa WhatsApp na ustaadhi ambaye aliwahi kutangaza kutaka kumuoa, jambo lililosababisha staa huyo kuamua kumfungulia mashtaka.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Wastara alifunguka kuwa kutokana na vitisho anavyotumiwa na ustadhi, hivyo akitua Dar kutoka mikoani atakwenda kumfungulia mashtaka kituo cha polisi kwani vitisho hivyo vinahatarisha usalama wake.
“Hebu fikiria mtu ananiandikia ujumbe kuwa atahakikisha nimeua ndiyo ataniacha, ina maana yale yanayonitokea ni yeye ananisababishia!” alisema Wastara.
Wastara alimtumia mwandishi ujumbe wa ustadhi huyo unaosomeka; ‘na bado siyo unatamani kuua na utaua, nitahakikisha umeua ndiyo na mimi nakuacha’.
Vitisho vya jamaa huyo vinakuja baada ya gazeti dada la hili, Ijumaa linalotikisa mitaani kila Ijumaa kuandika habari ya Wastara iliyosikitisha ambayo staa huyo alielezea namna anavyopatwa na hasira na kutaka kuua mtu ndipo ustadhi huyo akamjibu kwa ujumbe huo.
Ustadhi huyo aliwahi kuripotiwa na gazeti ndugu na hili, Risasi kuwa ana tatizo la kumsema Wastara hata awapo katikati ya swala, jambo lililomfanya awatafute waandishi ili wamsaidie kumuunganisha na mwigizaji huyo akitaka kumuoa lakini mwanadada huyo alidaiwa kumtolea nje.
GPL
No comments:
Post a Comment