Arusha.
Mwanasiasa mkongwe na miongoni mwa waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru leo amehutubia katika jukwaa la kampeni za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kusema chama tawala kimeishiwa pumzi.
Katika mkutano wa kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa katika viwanja vya Sinoni, mkoani Arusha, Kingunge amesema wale wote wanaohoji uamuzi wake wa kuihama CCM atawajibu hivi karibuni.gusa hapa kwa picha zaidi na video
Huku akijinadi kuwa ni mwanabadiliko tangu kuasisiwa kwa CCM, mwanasiasa huyo mkongwe nchini amesema sababu zinazoonyesha kuwa chama tawala kimeishiwa pumzi ni kudorora kwa uchumi ambao kwa sasa unakuwa chini ya asilimia saba.
“Hivi karibuni hasa awamu hii ya sasa kuna dalili kuwa baada ya CCM kukaa madarakani kwa nusu karne sasa imeanza kuishiwa pumzi. Rais Kikwete amerithi uchumi ukiwa unakuwa kwa asilimia saba…sasa kwa mujibu wa serikali yenyewe unakuwa kwa chini ya asilimia saba. Uchumi sasa unadorora.”
Baada ya kushuka jukwaani, mgombea urais Edward Lowassa alipanda jukwaani na kuwataka wananchi wasichelewe kumpa kura ili akashughulikie matatizo yanayowakabili ikiwemo afya, elimu, kuboresha mazingira ya biashara na kukuza kipato cha wananchi.
Lowassa amesema atahakikisha Tanzania inaendesha kilimo cha umwagiliaji na kutoa uhuru kwa wakulima kuuza mazao yote kokote atapopenda tofauti na hali ilivyo sasa.GUSA HAPA KWA HABAR ZAIDI.
No comments:
Post a Comment