Friday, October 23, 2015

JUA JINSI YA KULINDA KURA YAKO HAPA.


Kura halali zitakazopigwa siku ya Jumapili kwa ajili ya
kuwachagua viongozi kwenye Uchaguzi Mkuu zinaweza kuharibika ikiwa hazitapigwa kwa usahihi na kuondoa utata..
Kura iliyoharibika ni ile ambayo:
1)Haina alama yoyote
2)Imepigwa kwa wagombea zaidi ya mmoja
3)Imeandikwa jina la mpiga kura
4)Alama imewekwa nje ya kisanduku cha picha ya mgombea
5)Haina muhuri wenye alama rasmi

KURA SAHIHI;
Yenye alama ya ‘v’ kwenye kisanduku
Yenye alama yoyote kwenye kisanduku/picha/ jina la mgombea

UTATA;
Kutakuwa na utata endapo utaweka alama iliyopitiliza kisanduku cha mgombea mmoja na kufika kwa mwingine. Epuka kuharibu kura. Kura yako, mustakabali wako

No comments: