Tuesday, October 13, 2015

FURAHA YA INGIA KWENYE FAMILIA YA JOHN LEGEND NA MKEWE CHRISSY TEIGEN.

        John Legend na mkewe Chrissy Teigen wanatarajia
kufungua ukurasa mpya wa maisha baada ya kutangaza rasmi kuwa ni wazazi watarajiwa.
Baada ya miaka miwili ya ndoa yao huku wakitafuta mtoto hatimaye mkewe ambaye ni mwanamitindo Chrissy Teigen ametangaza rasmi kuwa ni mjamzito.
Katika ukurasa wake wa @Instagram Chrissy amesema wanayofuraha kutangaza kuwa ni mjamzito, na wengi walikua wakifahamu kuwa walikuwa wakijaribu kupata mtoto bila mafanikio, wanashukuru sasa wamefanikiwa.
Wawili hao walianza uhusiano mwaka 2007 na kuamua kufunga ndoa Septemba 2013.

No comments: