Saturday, October 24, 2015

MAMBO YA NAYO SABABISHA KUHARIBIKA KWA MIMBA.

   
         BILA shaka msomaji wangu utakuwa mzima wa afya
kama kawaida yetu katika ukurasa huu tumekuwa tukijuzana kuhusu elimu ya afya.Wiki iliyopita tulikuwa tukiangalia suala la kuharibika kwa ujauzito, na tulizungumzia ukubwa wa tatizo na tukaangalia baadhi ya vyanzo vya tatizo husika.
Leo tutaendelea na vyanzo vingine vinavyosababisha kuharibika kwa ujauzito.>>>TAZAMA HAPA KWA MARA YA KWANZA MIMBA IKIWA INA HARIBIKA<<<
Mbali na mimba zinazotolewa kiharamu, wanawake wengi mimba zao huharibika na moja ya sababu kubwa inayosabisha kuharibika kwa ujauzito ni maumbile ya kurithi. Wanawake wengi wenye tatizo hili wana vinasaba ambavyo si vya kawaida na kwa hiyo kiumbe kinakuwa katika hali ambayo kwa asili mimba haiwezi kukua na kama itakua na mtoto kuzaliwa basi mtoto huyo atakuwa na matatizo ya ajabu ya kimaumbile na akili.
Ni kwa sababu hiyo mimba huharibika na kutoka yenyewe.
Sababu nyingine ni kutokukua kwa yai lililorutubishwa. Katika uumbaji yai hukutana na mbegu ya mwanaume na mchakato wa kiumbe kukua huanza kwa yai kujitenga mara mbili.Upande mmoja hutengeneza kondo la nyuma na kifuko cha kutunza maji na sehemu ya pili hutengeneza kiumbe au mtoto. Hapa hutokea sehemu ya kondo la nyuma ikiendelea kukua wakati sehemu ya mtoto haikui kabisa.
Katika hali kama hiyo mwanamke hujikuta anapoteza ujauzito.Pia tatizo lingine linalosababisha mwanamke kuharibikiwa na ujauzito ni uvutaji wa sigara na msongo wa mawazo na unywaji wa pombe kupita kiasi wakati wa ujauzito huchangia mimba kuharibika.
Vilevile msongo wa mawazo na ukosefu wa lishe huchangia kwa kiasi kikubwa uharibikaji wa ujauzito. Mwanamke anapokuwa na msongo wa mawazo huathiri mfumo wa ukuaji wa kiumbe tumboni. Magonjwa yanayoathiri mwili wa mama tumboni kama vile malaria, kaswende, na kadhalika. Vyote hivi vina mchango mkubwa katika kuharibika kwa ujauzito.
Ikiwa mwanamke anakumbwa na changamoto za kuharibikiwa na ujauzito ni muhimu kujitathimini ili kujua chanzo cha tatizo ili aweze kupata matibabu. Mazingira kama haya kama mama hajafanya vipimo vinavyoweza kuangalia moja kwa moja, anaweza kuendelea kujidanganya kama ni mjamzito kwani kipimo cha mkojo kinaweza kuendelea kuonyesha kuwa mama ni mjamzito.
Hata hivyo bado ujauzito utapotea kabla ya wiki ya 24.
Dalili za mwanamke kujua kuwa ujauzito wake umeharibika
Mwanamke mwenye dalili zifuatazo na alikuwa na ujauzito basi atambue huenda ujauzito umeharibika. Dalili za mimba kuharibika zinaanza na mjamzito kutokwa na matone ya damu na kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu. Wajawazito wengine wanaweza kutokwa na damu bila kuhisi maumivu ya tumbo kabisa.
Wanawake wengi huenda ni kwa uelewa mdogo au dharau na hupuuza dalili za kutokwa damu hasa kama ni kidogo huchelewa kwenda kumuona daktari na matokeo yake mimba huharibika wakati angeweza kuzuilika.
Iwapo mimba zinatoka bila kuwa na sababu inayojulikana unatakiwa ufanyiwe uchunguzi wa magonjwa ya kurithi na magonjwa mengine yanayosababisha mimba kuharibika.
Matibabu ya kuharibika kwa mimba yanapatikana iwapo utawahi kufanyiwa uchunguzi ili upate tiba kulingana na tatizo lako pamoja na ushauri. Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya, nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume, unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.

No comments: