Wednesday, October 14, 2015

RUFUFU MKANDALA AFARIKI DUNIA.


RIP:- Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mkandala Rufufu aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa kutafsiri filamu za lugha mbalimbali kiingereza, kihindi, kichina, na hata wakati mwingine kifilipino yote aliyafanya kwenda katika lugha mama ya kiswahili, tutamisi zile mbwembwe, fix, uwongo uwongo wenye maana, mikogo ya sauti al-muradi kunogesha sikio la mtazamaji.

Rufufu amefariki dunia jana usiku wakati akitoka nyumbani kwake kuelekea harusini ambapo kwa mujibu wa wasimuliaji wanasema kuwa presha ilimpanda ghafla akaanguka na watu waliokuwa karibu naye walimkimbiza hospitalini na kabla hajapata matibabu akawa tayari amefariki dunia.

Dah tulifaidi sana tafsiri za filamu ulizokuwa unafanya hasa tuwapo safarini Tz ndani ndani, (wilayani, vijijini, mkoa kwa mkoa).

Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Rufufu mahala pema peponi. Amin

No comments: