Tuesday, October 13, 2015

SHILOLE HIYO MIMBA AU SHIBE?

SHILOLE390
       KITUMBO cha mwigizaji Zuwena Mohamed ‘Shilole’,  kimezua minong’ono ya aina yake kutoka kwa mashabiki na mastaa mbalimbali na kuwafanya wengi wao wabaki wakibishana kuwa mrembo huyo atakuwa katundikwa ujauzito na mchumba wake Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni nyumbani kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’,  aliyekuwa akisherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa ndipo wambeya walipoanza kumsengenya Shilole chinichini.
“Huyu atakuwa kanasa si bure,” alisikika mmbeya mmoja ambaye hakujitambulisha.
Alipoulizwa Shilole kama ni kweli amenasa ‘kibendi’, alijibu:
“Jamani sina mimba, watu watambue tu kwamba hiyo picha nilikuwa nimetoka kula, lakini pia wajue kwamba siku nikipata mimba watajua tu maana nitapiga picha za kutosha,” alisema Shilole

No comments: