Mahakama Kuu ya Tanzania, imehairisha kesi
namba 37 ya mwaka huu, ya mlalamikaji kuiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo.>>>GUSA HAPA KUTAZAMA VIDEO KAMILI <<<
Jopo hilo la majaji linaloongozwa na Jaji Sakieti Kihiyo pamoja na Lugano Mwandambo na Aloysius Mjujulizi limeahirisha kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mgombea ubunge Viti Maalum kupitia Chadema, Ammy Kibatala..>>>GUSA HAPA KUTAZAMA VIDEO KAMILI <<<
Kesi hiyo sasa itasikilizwa kesho saa 3 asubuhi baada ya upande wa serikali kudai kuwa walikuwa hawajamaliza kujibu hoja au kuweka pingamizi sababu walipokea notisi ya walalamikaji muda wa jioni hivyo hawakujiandaa..>>>GUSA HAPA KUTAZAMA VIDEO KAMILI <<<
“Mheshimiwa Jaji, tunaomba tupewe muda kwani tulipokea nyaraka hizi muda wa kazi ukiwa umekaribia kwisha hivyo hatukujiandaa, tunaomba tupewe muda kama ikiwezekana tulete majibu saa 8:30 Mchana leo kama mahakama itaona inapendeza,” alisema Wakili wa Serikali Obadia Kameya..>>>GUSA HAPA KUTAZAMA VIDEO KAMILI <<<
Kabla Majaji hawajatolea uamuzi ombi hilo walimshauri Wakili wa mlalamikaji, Peter Kibatala kubadilisha mashtaka na kumshtaki Mkurugenzi wa Uchaguzi kwani ndiye mtendaji mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi badala ya Mwenyekiti wa Tume hiyo.
.>>>GUSA HAPA KUTAZAMA VIDEO KAMILI <<<
No comments:
Post a Comment