Sunday, October 11, 2015

OBAMA AMPA KANYE WEST AKIBA YA MANENO JUU YA SWALA LAKE LA KUGOMBEA URAISI.


Hivi karibuni rapper wa Marekani Kanye West alitangaza nia yake ya kutaka kuingia ikulu ya Marekani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2020.

Alitangaza nia yake hiyo wakati wa tuzo za VMA.
Rais wa Marekani Barack Obama amemshauri rapper huyo kuhusu uamuzi wake huo wakati wa alipohudhuria uchangishaji wa fedha wakati wa speech yake  iliyofanyika jana Oktoba 10 wakati Kanye West naye akiwa mmoja wa waliohudhuria.
Kwanza Obama alishangazwa na uamuzi wa Kanye West kuwania nafasi hiyo na pia hakuwa na cha kumshauri kuhusu uamuzi wake huo.
Ingawa amemtaka kama Rais atumie muda mwingi kufanya maamuzi kwa sababu kuna watu wengi ambao wana tabia za ajabu hivyo anapaswa kukubaliana nao ili aweze kumudu nafasi yake.
Pia alimuuliza kama anafikiri tena Wamarekani watampa Mmarekani mweusi nafasi ya kuwaongoza kama ilivyokuwa kwake.
Obama na Kanye West wote wametokea katika jimbo la Chicago Kusini  
          

No comments: