Sikuchache zilizo pita ndani ya wiki hii, watu wasio na nia njema walitengeneza mfano wa gazeti la Mwananchi
kwenye mitandao ya kijamii likionyesha habari ya kumchafua Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja wa vyama vinavyounda Ukawa, James Mbatia.
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen, imelaani vikali upotoshaji wa makusudi unaolenga kutumia jina la Mwananchi kuwachafua wanasiasa na watu wengine hasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Mapema wiki hii, watu wasio na nia njema walitengeneza mfano wa gazeti la Mwananchi kwenye mitandao ya kijamii likionyesha habari ya kumchafua Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja wa vyama vinavyounda Ukawa, James Mbatia. Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu alishauri timu za kampeni za vyama vyote, kunadi sera zao na kuonyesha jinsi watakavyozitimiza badala ya kusambaza propaganda zinazolenga kuchafua jina la kampuni ya Mwananchi. Alisema MCL inapanga kuwasilisha malalamiko rasmi kwa vyombo vya sheria ili vichukue hatua kutokana na udhalilishaji huo.
Hii si mara ya kwanza kwa watu wenye nia mbaya na magazeti ya kampuni ya Mwananchi kutengeneza mfano wa gazeti na kuandika vichwa vya habari ambavyo vina lengo la kuichafua.
Machumu alisema ingawa MCL haihusiki kwa vyovyote vile na gazeti feki hilo lililokuwa linasambaa kwenye mitandao, inamuomba radhi Mbatia na wengine wote walioumizwa na kitendo hicho
No comments:
Post a Comment