Mwili wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda aliyefariki juzi katika hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu, umewasili leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Emirates.
Mwili wa Waziri Kigoda utaagwa kesho viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment