|
Hii ni picha ya vijana wa Tanzania waliyo kuwa wanalazimishwa kurudi Tanzania ili hali polisi waliyo kuwa waki wakamata wanachukua kila kitu walicho nacho nakuweka mifukoni mwao yani simu,pesa na chochote
watakacho kukuta nacho, kiu kweli hawa raia hawa kutendewa haki hata kidogo baadhi ya viongozi wa taifa la Mozambique walijikosha kwakusema raia hao wanakaa machimboni hiyo siyo kweli Montepuez siyo sehemu ya machimbo ni mji wakuishi watu na hata nyumba ya mama wa moja ya viongozi was nyanda ya juu kabisa ya serikali ipo hapa montepuez pia kuna soko kubwa tu ambalo asilimia kubwa ya watu wenye maduka ni watanzania na wa west 95% na hawa wenye maduka siyo kama wamepangishwa wengi wanakuwa wameyanunua kabisa haya maduka. |
|
Polisi wakiwa kwenye msako |
Hili jambo lime wauma watu wengi sana kiukweli ni bora lingetolewa tangazo kwamba wageni wote mnatakiwa muondoke lakini wao wamekuja na kuvamia kupola ,kuiba,kunyang'anya ,kubaka Dada zetu, wamelizalilisha sana taifa letu kiukweli haya matukio ukiwa mbali hutoguswa sana Ila ungeshuhudia ndugu msomaji ungelia na kuingiwa na roho ya kikatili sana, kwa mfano kuna binti anaitwa Marian ni mtanzania mapolisi wameenda kuvunja kwenye nyumba yao nakuingia ndani wakawakuta wamelala sababu ya uzuri wa huyu binti polisi wakaanza kumuingilia kinguvu hii imetokea maeneo ya Montepuez na binti huyu ni moja ya mabinti waliyo ojiwa na waandishi kadhaa na kuelezea tukio zima, acha Montepuez ukiongelea Nanhupu ndiyo matukio mengi sana yakinyama yametendeka kuna binti ni wa Arusha kabakwa mpaka kupoteza maisha, huko huko nanhupu mtuna mke wake wamelala usiku waka waingilia askari wakaanza kumbaka mke kisha wakamwambia mume alete beseni LA maji ili awasafishe tupu zao huu ni udhalilifu ulioje?
Kwa picha na habari zaid penda kuwa mtembezi wa hii blog Mara kwa Mara.
No comments:
Post a Comment