Kufuatia
madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekuwa na katabia
ka’ kujiweka kimahaba kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakati Zarinah Hassan
‘Zari’ akiwa Sauzi, madai yametua mezani mwa gazeti hili kuwa, kimenuka
kati ya Zari na Kajala.
>>>>INGIA HAPA KWA HABARI NYINGI ZAIDI,<<<<<
>>>>INGIA HAPA KWA HABARI NYINGI ZAIDI,<<<<<
Chanzo
chetu makini ambacho kimeomba jina lake lisitajwe gazetini kimedai
kuwa, hivi karibuni baada ya Zari kupata ubuyu huo wa kuchovyewa penzi
lake, alitafuta simu ya Kajala kisha kumpigia na kumpa makavu kuwa,
asimuingilie kwenye himaya yake.
“Siku
moja nilikuwa na Kajala, mara ikaingia simu ambapo alipopokea akasikia
sauti ya Zari, basi unaambiwa akamsema sana juu ya kuingilia penzi lake,
Kajala akawa kimyaa, wala hajajibu lolote, inavyoonekana alipewa
makavu,” alidai mtoa habari huyo.
Baada
ya kupata habari hiyo, paparazi wetu alimtafuta Kajala ili kuzungumzia
madai hayo ambapo alipokea simu na kupewa mkanda mzima, alishangaa na
kuuliza: “Nyie nani kawaletea hizo habari, jamani watu wambeya sana.”
Alipobanwa zaidi akasema hawezi kuongelea hayo mambo.
Zari
hakuweza kupatikana mara moja ila Ijumaa lilifanya jitihada za
kumtafuta Diamond kupitia simu yake ambapo mahojiano yalikuwa kama
ifuatavyo:
Ijumaa:
Ebwana kuna habari kuwa Zari alimpiga mkwara Kajala juu ya tuhuma za
kutoka na wewe kimapenzi sijui hilo likoje kwa upande wako?
Diamond: Hahahaa, sema nini mwanangu, hapa sikusikii vizuri nipo njiani naelekea Sweden.
Ijumaa: We nijibu tu, imekuwaje?
Diamond: Dah!
Kweli mimi hata nakosa hata la kusema hapo maana mambo ya wanawake ni
ngumu kuyaingilia kwa namna yoyote ile ila sijui nini hapo.
Ijumaa: Oke poa.
Kipindi
cha nyuma ilidaiwa kuwa, Kajala alikuwa na uhusiano wa siri na Diamond
mpaka ikafikia hatua baadhi ya watu kuhisi hata ile mimba aliyokuwa nayo
Kajala ilikuwa ya msanii huyo anayefanya poa kwa sasa kwenye muziki.
No comments:
Post a Comment