Huenda ukawa umezoea na kuboreka na foleni ya jiji la Dar Es Salaam ambalo wakati mwingine inaweza kukugharimu kwa zaidi ya saa moja kukaa katika foleni kutoka Tegeta hadi Posta, hususani
mvua ikiwa inanyesha Dar Es Salaam sehemu huwa zinakuwa na foleni kubwa. Mtu wangu wa nguvu nimekutana na list ya mpya kutoka www.telegraph.co.uk ya miji 10 inayoongoza kwa foleni Duniani, imeandikwa 04/02/2016.
mvua ikiwa inanyesha Dar Es Salaam sehemu huwa zinakuwa na foleni kubwa. Mtu wangu wa nguvu nimekutana na list ya mpya kutoka www.telegraph.co.uk ya miji 10 inayoongoza kwa foleni Duniani, imeandikwa 04/02/2016.
10- Los Angels huu ni mji ambao alikuwa anaishi King of Pop Michael Jackson, huu ndio mji wa 10 unaoongoza kwa foleni duniani, licha ya kuwa miundombinu yake ya viwango vya juu.
9- Shenzhen ni moja kati ya miji ya China
inayoongoza kwa kukua kwa kasi una watu zaidi ya milioni 10, lakini
ukuaji wa miji hiyo haujaishia katika maendelea ya kawaida tu, lakini
huu unatajwa kuwa mji namba 9 unaoongoza kwa foleni duniani.
8- Rio de Janeiro Brazil,
mji huu unatajwa kuwa namba nane kwa kuongoza katika foleni duniani,
lakini huu ni mji ambao ukuaji wake umeongezeka baada ya kufanyika kwa
michuano ya Kombe la Dunia 2014
7- Mji mkuu wa Romania Bucharest
ni moja kati ya miji iliyoingia kwenye headlines ya kuongoza kuwa na
foleni, kwa mujibu wa takwimu ya mwaka, inataja kuwa muda wa saa 94 kwa
mwaka, magri hutumia kukaa kwenye foleni pekee.
6- Mji wa Recife licha ya kuwa sio maarufu Brazil kuliko Rio de Janeiro, lakini ndio mji unaoongoza kwa foleni kutoka America ya Kusini.
5- Chongqing huu ni mji wa pili kutoka China kutajwa kuongoza kuwa na foleni katika list hii, population ya watu waliopo katika mji huo imekuwa mara zaidi tangu mwaka 1990.
4- Mexico City huu ni mji namba nne kwa kuwa na foleni duniani, ni kawaida kwa mtu kukaa katika foleni kwa wastani wa dakika 30 hadi 58.
3- St Petersburg hii
ni moja kati ya miji mizuri iliyopo Urusi, sifa kubwa ya mji huu ni kuwa
una foleni kubwa sana, hivyo kama ni mgeni unaweza kushangazwa na hili.
2- Ukiachana na mji wa St Petersburg uliopo Urusi, haina maana kuwa huo ndio mji pekee wa Urusi unaoongoza kwa Moscow ndio kiboko ya miji yote ya Urusi, unaongoza kuwa na foleni.
1- Istanbul Uturuki ndio mji pekee unaoongoza kwa foleni duniani, unatajwa gari ukaa foleni kwa wastani wa saa 125 kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment